Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 3:1-5

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Kuanguka Kwa Mwanadamu

1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao Bwana Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, "Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?"

2 Mwanamke akamjibu nyoka, "Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini, 3 lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala kuugusa, la sivyo mtakufa.’ "

4 Lakini nyoka akamwambia mwanamke, "Hakika hamtakufa. 5 Kwa maana Mungu anajua ya kuwa wakati mtakapoyala, macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Basi nyoka alikuwa mjanja kuliko wanyama pori wote ambao Bwana Mwenyezi Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, "Ati Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?"

    2 Mwanamke akamjibu nyoka, "Tunaweza kula matunda ya miti iliyo katika bustani, 3 lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala kuugusa, la sivyo mtakufa.’ "

    4 Lakini nyoka akamwambia mwanamke, "Hakika hamtakufa. 5 Kwa maana Mungu anajua kwamba mtakapokula tunda hilo, macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Mt 10:16;Ufu 12:2,9;20:2Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? 2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; 3 Mwa 2:16,17lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. 4 2 Kor 11:3;1 Tim 2:14Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.