Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 37:5,7,9,24,28,31,33

5 Yosefu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi. 7 Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani, ghafula mganda wangu ukasimama wima, wakati miganda yenu ikiuzunguka na kuuinamia."

9 Kisha akaota ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake akisema, "Sikilizeni, nimeota ndoto nyingine, wakati huu jua, mwezi na nyota kumi na moja zilikuwa zinanisujudia."

24 Kisha wakamchukua wakamtupa katika shimo. Wakati huo shimo lilikuwa tupu, halikuwa na maji ndani yake.

28 Kwa hiyo wale wafanyabiashara Wamidiani walipofika pale, ndugu zake wakamtoa Yosefu kutoka kwenye lile shimo, na kumuuza kwa shekeli ishirini37:28 Shekeli 20 ni sawa na gramu 200. za fedha kwa wale Waishmaeli, ambao walimpeleka Misri.

31 Kisha wakalichukua lile joho la Yosefu, wakachinja mbuzi na kulichovya katika damu.

33 Baba yao akalitambua akasema, "Hili ni joho la mwanangu! Mnyama mkali amemrarua. Hakika Yosefu ameraruliwa vipande vipande."

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.