12 Utakapoilima ardhi, haitakupa tena mazao yake. Utakuwa mtu wa kutangatanga duniani asiye na utulivu."
13 Kaini akamwambia Bwana, "Adhabu yangu ni zaidi ya niwezavyo kustahimili. 14 Leo unanifukuza kutoka nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga asiyetulia duniani na yeyote anionaye ataniua."
15 Lakini Bwana akamwambia, "La sivyo, ikiwa mtu yeyote atamuua Kaini atalipizwa kisasi mara saba zaidi." Kisha Bwana akamwekea Kaini alama ili mtu yeyote ambaye angemwona asimuue. 16 Kwa hiyo Kaini akaondoka mbele za Bwana akaenda kuishi katika nchi ya Nodi, iliyoko mashariki ya Edeni.