Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 8:15-19

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

15 Ndipo Mungu akamwambia Noa, 16 "Toka ndani ya safina, wewe na mkeo na wanao na wake zao. 17 Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe: Ndege, wanyama na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia."

18 Kwa hiyo Noa akatoka nje pamoja na mkewe, wanawe na wake zao. 19 Wanyama wote na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi na ndege wote, kila kitu kiendacho juu ya nchi, aina moja baada ya nyingine vikatoka katika safina, kila aina ya kiumbe, kimoja baada ya kingine.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    15 Ndipo Mungu akamwambia Nuhu, 16 "Toka katika safina, wewe na mkeo, na wanao na wake zao. 17 Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe, wakiwamo ndege, wanyama na viumbe vyote vinavyotambaa ardhini, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia."

    18 Kwa hiyo Nuhu akatoka nje pamoja na mkewe, na wanawe na wake zao. 19 Wanyama wote na viumbe vyote vinavyotambaa ardhini, na ndege wote, kila kitu kinachoenda juu ya nchi, aina moja baada ya nyingine vikatoka katika safina.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    15 Mungu akamwambia Nuhu, akisema, 16 Mwa 7:13;Zab 121:8Toka katika safina, wewe, na mkeo, na wanao, na wake za wanao pamoja nawe. 17 Mwa 1:22Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi. 18 Basi Nuhu akatoka, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; 19 kila mnyama, na kila kitambaacho, na kila ndege, kila kinachokwenda juu ya nchi kwa makabila yao, wakatoka katika safina.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.