16 Kwa habari ya wosia,9:16 Wosia hapa kwa neno la Kiyunani ni agano. ni muhimu kuthibitisha kifo cha yule aliyeutoa, 17 kwa sababu wosia huwa na nguvu tu wakati mtu ameshakufa; kamwe hauwezi kutumika wakati yule aliyeuandika bado yuko hai. 18 Hii ndiyo sababu hata lile agano la kwanza halikuweza kutekelezwa pasipo damu. 19 Mose alipotangaza kila amri kwa watu wote, alichukua damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji, sufu nyekundu na matawi ya mti wa hisopo, akanyunyizia kile kitabu na watu wote. 20 Alisema, "Hii ndiyo damu ya agano, ambalo Mungu amewaamuru kulitii."