Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 1

45 Filipo naye akamkuta Nathanaeli na kumwambia, "Tumemwona yeye ambaye Mose aliandika habari zake katika Sheria na ambaye pia manabii waliandika kumhusu, yaani, Yesu wa Nazareti, mwana wa Yosefu."

46 Nathanaeli akauliza, "Nazareti! Je, kitu chochote chema chaweza kutoka Nazareti?" Filipo akamwambia, "Njoo uone."

47 Yesu alipomwona Nathanaeli anakaribia, akanena habari zake akasema, "Tazama huyu ni Mwisraeli kweli kweli; hana hila ndani yake."

48 Nathanaeli akamuuliza, "Umenifahamuje?"

Yesu akamjibu, "Nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita."

49 Nathanaeli akamwambia, "Rabi, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!"

50 Yesu akamwambia, "Unaamini kwa kuwa nilikuambia nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini? Basi utaona mambo makuu zaidi kuliko hilo." 51 Ndipo akawaambia, "Amin, amin nawaambia, ninyi mtaona mbingu ikifunguka na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu."

Veja também