Pular para o conteúdo
Publicidade

João 11

21 Martha akamwambia Yesu, "Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa. 22 Lakini sasa ninajua kuwa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa."

23 Yesu akamwambia, "Ndugu yako atafufuka."

24 Martha akamjibu, "Ninajua ya kuwa atafufuka wakati wa ufufuo wa wafu siku ya mwisho."

25 Yesu akamwambia, "Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi 26 na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?"

27 Martha akamwambia, "Ndiyo Bwana, ninaamini ya kuwa wewe ndiwe Kristo,11:27 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Mwana wa Mungu, yeye ajaye ulimwenguni."

Veja também