Kuingia Kwa Yesu Yerusalemu Kwa Ushindi
12 Siku iliyofuata umati mkubwa uliokuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Yesu angekuja Yerusalemu. 13 Basi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema,
"Hosana!"12:13 Kiebrania kusema Okoa, basi likawa neno la shangwe.
"Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!"
"Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!"