4 Pilato akatoka tena nje akawaambia wale waliokusanyika, "Tazameni, namkabidhi Yesu kwenu kuwajulisha kwamba mimi sikumwona ana hatia." 5 Kwa hiyo Yesu akatoka nje akiwa amevaa ile taji ya miiba na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, "Tazameni, huyu hapa huyo mtu!"
6 Wale viongozi wa makuhani na maafisa walipomwona, wakapiga kelele wakisema, "Msulubishe! Msulubishe!"
Pilato akawaambia, "Mchukueni ninyi mkamsulubishe, mimi sioni hatia juu yake."