Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 20:1,6,7,11,14-16,18

Kufufuka Kwa Yesu

1 Alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma, kulipokuwa kungali giza bado, Maria Magdalene alikwenda kaburini na kukuta lile jiwe limeondolewa penye ingilio.

6 Ndipo Simoni Petro akaja, akimfuata nyuma akaenda moja kwa moja hadi ndani ya kaburi. Naye akaona vile vitambaa vya ile sanda vikiwa pale chini 7 na kile kitambaa kilichokuwa kichwani mwa Yesu. Kitambaa hicho kilikuwa kimekunjwa mahali pa peke yake, mbali na vile vitambaa vya kitani vya ile sanda.

11 Lakini Maria Magdalene akasimama nje ya kaburi akilia. Alipokuwa akilia, akainama, kuchungulia mle kaburini,

14 Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Yesu amesimama, lakini hakumtambua.

15 Yesu akamwambia, "Mwanamke, mbona unalia? Unamtafuta nani?"

Maria akidhani ya kuwa aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akamwambia, "Bwana, kama ni wewe umemchukua, tafadhali nionyeshe ulikomweka, nami nitamchukua."

16 Yesu akamwita, "Maria!"

Ndipo Maria akamgeukia Yesu na kusema naye kwa Kiebrania, "Rabboni!" (maana yake Mwalimu).

18 Kwa hiyo Maria Magdalene akaenda kuwatangazia wanafunzi wa Yesu, akisema, "Nimemwona Bwana!" Naye akawaambia kwamba Yesu alikuwa amemweleza mambo hayo yote.

Yesu Awatokea Wanafunzi Wake

(Mathayo 28:16-20; Marko 16:14-18; Luka 24:36-49)

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.