Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 20:11,14-18

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

11 Lakini Maria Magdalene akasimama nje ya kaburi akilia. Alipokuwa akilia, akainama, kuchungulia mle kaburini,

14 Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Yesu amesimama, lakini hakumtambua.

15 Yesu akamwambia, "Mwanamke, mbona unalia? Unamtafuta nani?"

Maria akidhani ya kuwa aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akamwambia, "Bwana, kama ni wewe umemchukua, tafadhali nionyeshe ulikomweka, nami nitamchukua."

16 Yesu akamwita, "Maria!"

Ndipo Maria akamgeukia Yesu na kusema naye kwa Kiebrania, "Rabboni!" (maana yake Mwalimu).

17 Yesu akamwambia, "Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ "

18 Kwa hiyo Maria Magdalene akaenda kuwatangazia wanafunzi wa Yesu, akisema, "Nimemwona Bwana!" Naye akawaambia kwamba Yesu alikuwa amemweleza mambo hayo yote.

Yesu Awatokea Wanafunzi Wake

(Mathayo 28:16-20; Marko 16:14-18; Luka 24:36-49)

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    11 Lakini Mariamu Magdalene akasimama nje ya kaburi akilia. Alipokuwa akilia, akainama kuchungulia mle kaburini,

    14 Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Isa amesimama, lakini hakumtambua.

    15 Isa akamwambia, "Mwanamke, mbona unalia? Unamtafuta nani?"

    Mariamu, akidhani alikuwa anaongea na mtunza bustani, akamwambia, "Bwana, kama ni wewe umemchukua, tafadhali nioneshe ulikomweka, nami nitamchukua."

    16 Isa akamwita, "Mariamu!"

    Ndipo Mariamu akamgeukia Isa na kusema naye kwa Kiebrania, "Raboni!" (maana yake "Mwalimu").

    17 Isa akamwambia, "Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba20:17 Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (Yohana 1:1-2), wa kiroho, bali si wa kimwili.. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ "

    18 Kwa hiyo Mariamu Magdalene akaenda kuwatangazia wanafunzi wa Isa, akisema, "Nimemwona Bwana!" Naye akawaambia kwamba Isa alikuwa amemweleza mambo hayo yote.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    11 Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Wakati alipokuwa akilia, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi. 14 Naye akiisha kusema hayo, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu. 15 Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa. 16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu). 17 Ebr 2:11,12;Rum 8:29Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu. 18 Mariamu Magdalene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba, Nimemwona Bwana, na ya kwamba amemwambia hayo.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.