14 Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Yesu amesimama, lakini hakumtambua.
15 Yesu akamwambia, "Mwanamke, mbona unalia? Unamtafuta nani?"
Maria akidhani ya kuwa aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akamwambia, "Bwana, kama ni wewe umemchukua, tafadhali nionyeshe ulikomweka, nami nitamchukua."
16 Yesu akamwita, "Maria!"
Ndipo Maria akamgeukia Yesu na kusema naye kwa Kiebrania, "Rabboni!" (maana yake Mwalimu).