Pular para o conteúdo
Publicidade

João 20

16 Yesu akamwita, "Maria!"

Ndipo Maria akamgeukia Yesu na kusema naye kwa Kiebrania, "Rabboni!" (maana yake Mwalimu).

17 Yesu akamwambia, "Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ "

18 Kwa hiyo Maria Magdalene akaenda kuwatangazia wanafunzi wa Yesu, akisema, "Nimemwona Bwana!" Naye akawaambia kwamba Yesu alikuwa amemweleza mambo hayo yote.

Veja também