Yesu Awatokea Wanafunzi Wake
19 Ikawa jioni ya ile siku ya kwanza ya juma, wanafunzi wake walikuwa pamoja, milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi. Naye Yesu aliwatokea, akasimama katikati yao, akasema, "Amani iwe nanyi!" 20 Baada ya kusema haya, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Wanafunzi wake wakafurahi sana walipomwona Bwana.
21 Yesu akawaambia tena, "Amani iwe nanyi! Kama vile Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawatuma ninyi." 22 Naye alipokwisha kusema haya, akawavuvia, akawaambia, "Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 Mkimwondolea mtu yeyote dhambi zake, zitaondolewa, na yeyote msiyemwondolea dhambi zake, hazitaondolewa."