Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 20:24-29

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Yesu Anamtokea Tomaso

24 Lakini Tomaso, aliyeitwa Didimasi, yaani Pacha, mmoja wa wale kumi na wawili, hakuwa pamoja nao Yesu alipokuja. 25 Hivyo wale wanafunzi wengine wakamwambia, "Tumemwona Bwana."

Lakini yeye akawaambia, "Nisipoona zile alama za misumari mikononi mwake, na kuweka kidole changu kwenye hizo alama za misumari na mkono wangu ubavuni mwake, sitaamini."

26 Baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwa tena pamoja ndani ya nyumba, naye Tomaso alikuwa pamoja nao. Ndipo Yesu akaja milango ikiwa imefungwa na kusimama katikati yao akasema, "Amani iwe nanyi." 27 Kisha akamwambia Tomaso, "Weka kidole chako hapa na uone mikono yangu, nyoosha mkono wako uguse ubavuni mwangu. Usiwe na shaka, bali uamini tu."

28 Tomaso akamwambia, "Bwana wangu na Mungu wangu!"

29 Yesu akamwambia, "Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    24 Lakini Tomaso (aliyeitwa Didimasi20:24 yaani Pacha), mmoja wa wale kumi na wawili, hakuwa pamoja nao Isa alipokuja. 25 Hivyo wale wanafunzi wengine wakamwambia, "Tumemwona Bwana Isa."

    Lakini yeye akawaambia, "Nisipoona zile alama za misumari mikononi mwake, na kuweka kidole changu kwenye hizo alama za misumari, na mkono wangu ubavuni mwake, sitaamini."

    26 Baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwa tena pamoja ndani ya nyumba, naye Tomaso alikuwa pamoja nao. Ndipo Isa akaja, milango ikiwa imefungwa, na kusimama katikati yao, akasema, "Amani iwe nanyi." 27 Kisha akamwambia Tomaso, "Weka kidole chako hapa na uone mikono yangu, nyoosha mkono wako uguse ubavuni mwangu. Usiwe na shaka, bali uamini tu."

    28 Tomaso akamwambia, "Bwana wangu na Mungu wangu!"

    29 Isa akamwambia, "Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    24 Yn 11:16;14:5Lakini mmoja wa wale Kumi na Wawili, Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu. 25 Yn 19:34Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo.

    26 Yn 20:19Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu. 27 Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye. 28 Yn 1:1Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! 29 1 Pet 1:8Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.