Kusudi La Kitabu Hiki
30 Yesu alifanya miujiza mingine mingi mbele za wanafunzi wake, ambayo haikuandikwa katika kitabu hiki. 31 Lakini haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo,20:31 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Mwana wa Mungu, na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.