Yesu Amuuliza Petro Kama Anampenda
15 Walipokwisha kula, Yesu akamuuliza Simoni Petro, "Je, Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?"
Yeye akamjibu, "Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda."
Yesu akamwambia, "Lisha wana-kondoo wangu."
19 Yesu alisema haya ili kuashiria ni kifo cha aina gani Petro atakachomtukuza nacho Mungu. Kisha Yesu akamwambia Petro, "Nifuate!"