Publicidade

João 4

46 Hivyo Yesu akaja tena mpaka Kana ya Galilaya, kule alikokuwa amebadili maji kuwa divai. Huko kulikuwepo na afisa mmoja wa mfalme, ambaye mwanawe alikuwa mgonjwa huko Kapernaumu. 47 Huyo mtu aliposikia kwamba Yesu alikuwa amewasili Galilaya kutoka Uyahudi, alimwendea na kumwomba ili aje kumponya mwanawe, aliyekuwa mgonjwa karibu ya kufa.

48 Yesu akamwambia, "Ninyi watu msipoona ishara na miujiza kamwe hamtaamini."

49 Yule afisa wa mfalme akamwambia, "Bwana, tafadhali shuka kabla mwanangu hajafa."

50 Yesu akamjibu, "Enenda zako, mwanao yu hai."

Yule afisa akaamini yale maneno Yesu aliyomwambia, akaondoka akaenda zake. 51 Alipokuwa bado yuko njiani, akakutana na watumishi wake wakamwambia kwamba mwanawe yu mzima. 52 Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, "Jana yapata saa saba, homa ilimwacha."

53 Ndipo baba wa huyo mtoto akakumbuka kuwa huo ndio wakati ambapo Yesu alikuwa amemwambia, "Mwanao yu hai." Kwa hiyo yeye pamoja na wote wa nyumbani mwake wakamwamini Yesu.

54 Hii ilikuwa ishara ya pili ambayo Yesu alifanya aliporudi Galilaya kutoka Uyahudi.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-