Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 4:7,9,10,16-18,26,29

7 Mwanamke mmoja Msamaria akaja kuteka maji, Yesu akamwambia, "Naomba maji ninywe."

9 Yule mwanamke Msamaria akamjibu, "Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?" (Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria.)

10 Yesu akajibu akamwambia, "Kama ungelijua karama ya Mungu, naye ni nani anayekuambia, Nipe maji ninywe, wewe ungelimwomba yeye, naye angelikupa maji yaliyo hai."

16 Yesu akamjibu, "Nenda ukamwite mumeo, uje naye hapa."

17 Yule mwanamke akajibu, "Sina mume."

Yesu akamwambia, "Umesema kweli kuwa huna mume. 18 Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano na mwanaume unayeishi naye sasa si mume wako! Umesema ukweli."

26 Yesu akamwambia, "Mimi ninayezungumza nawe, ndiye."

29 "Njooni mkamwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda! Je, yawezekana huyu ndiye Kristo?"4:29 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.