7 Mwanamke mmoja Msamaria akaja kuteka maji, Yesu akamwambia, "Naomba maji ninywe."
9 Yule mwanamke Msamaria akamjibu, "Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?" (Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria.)
26 Yesu akamwambia, "Mimi ninayezungumza nawe, ndiye."
27 Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemuuliza, "Unataka nini kwake?" Au "Kwa nini unazungumza naye?"
Wasamaria Wengi Waamini
39 Wasamaria wengi katika mji ule wakamwamini Yesu kwa sababu ya ushuhuda wa yule mwanamke alipowaambia kwamba, "Ameniambia kila kitu nilichotenda."