Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 6:35,48,51,53,56,60,66

35 Yesu akawaambia, "Mimi ndimi mkate wa uzima. Yeye ajaye kwangu, hataona njaa kamwe na yeye aniaminiye, hataona kiu kamwe.

48 Mimi ni mkate wa uzima. 51 Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu yeyote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu."

53 Hivyo Yesu akawaambia, "Amin, amin nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 56 Yeyote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake.

Wafuasi Wengi Wamwacha Yesu

60 Wengi wa wafuasi wake waliposikia jambo hili wakasema, "Mafundisho haya ni magumu. Ni nani awezaye kuyapokea?"

66 Tangu wakati huo wafuasi wake wengi wakarejea nyuma wakaacha kumfuata.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.