Pular para o conteúdo
Publicidade

João 6

5 Yesu alipotazama na kuuona ule umati mkubwa wa watu ukimjia, akamwambia Filipo, "Tutanunua wapi mikate ili watu hawa wale?" 6 Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya.

7 Filipo akamjibu, "Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili,6:7 Dinari 200 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 200; mshahara wa kibarua ulikuwa dinari moja kwa siku. hazitoshi kununua mikate ya kuwapa watu hawa ili kila mtu apate kidogo."

Veja também