Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 8:41,42,44

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

41 Ninyi mnafanya mambo afanyayo baba yenu."

Wakamjibu, "Sisi hatukuzaliwa kwa uzinzi. Tunaye Baba mmoja, Mungu pekee."

42 Yesu akawaambia, "Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda, kwa maana nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, ila yeye alinituma. 44 Ninyi ni watoto wa baba yenu ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    41 Ninyi mnafanya mambo afanyayo baba yenu."

    Wakamjibu, "Sisi hatukuzaliwa kwa uzinzi. Tunaye Baba mmoja, Mungu pekee."

    42 Isa akawaambia, "Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda, kwa maana nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, ila yeye alinituma. 44 Ninyi ni watoto wa baba yenu, ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli, maana hamna kweli ndani yake. Anaposema uongo, yeye husema lugha yake ya asili kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    41 Mwa 3:15;Kum 23:2Ninyi mnazitenda kazi za baba yenu. Ndipo walipomwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zinaa; sisi tunaye Baba mmoja, yaani, Mungu. 42 1 Yoh 5:1Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi; kwa maana nilitoka kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma. 44 1 Yoh 3:8-10;Mwa 3:4;2 Pet 2:4Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa uongo.8:44 Kigiriki ni ‘wa huo’.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.