21 na kusema:
"Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi,
nami nitaondoka uchi,1:21 Au: nitarudi huko uchi.
Bwana alinipa, naye Bwana ameviondoa,
jina la Bwana litukuzwe."
22 Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi kwa kumlaumu Mungu kwa kufanya ubaya.