9 Mke wake akamwambia, "Je, bado unashikamana na uadilifu wako? Mlaani Mungu nawe ukafe!"
10 Akamjibu, "Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavu2:10 Mpumbavu hapa ina maana ya kupungukiwa maadili. yeyote angenena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?"
Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi katika kusema kwake.