Kuzaliwa Kwa Yesu Kwatabiriwa
26 Mwezi wa sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alimtuma malaika Gabrieli aende Galilaya katika mji wa Nazareti, 27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu mmoja jina lake Yosefu wa nyumba ya Daudi. Jina la huyu mwanamwali bikira ni Maria. 28 Naye malaika akaja kwake akamwambia: "Salamu, wewe uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!"
36 Tazama, jamaa yako Elizabeti amechukua mimba katika uzee wake, na huu ni mwezi wake wa sita, yeye aliyeitwa tasa.
38 Maria akasema, "Tazama, mimi ni mtumishi wa Bwana. Na iwe kwangu kama ulivyosema." Kisha malaika akaondoka, akamwacha.
Maria Aenda Kumtembelea Elizabeti
39 Wakati huo Maria akajiandaa, akaharakisha kwenda katika mji mmoja kwenye vilima vya Uyahudi.
56 Maria akakaa na Elizabeti karibu miezi mitatu, kisha akarudi nyumbani kwake.