Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 13:12-16

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

12 Yesu alipomwona, akamwita, akamwambia, "Mwanamke, uwe huru, umepona ugonjwa wako." 13 Yesu alipomwekea mikono yake, mara akasimama wima akaanza kumtukuza Mungu.

14 Lakini kiongozi wa sinagogi akakasirika kwa sababu Yesu alikuwa ameponya mtu siku ya Sabato. Akaambia ule umati wa watu, "Kuna siku sita ambazo watu wanapaswa kufanya kazi. Katika siku hizo, njooni mponywe, lakini si katika siku ya Sabato."

15 Lakini Bwana akamjibu, "Enyi wanafiki! Je, kila mmoja wenu hamfungulii ngʼombe wake au punda wake kutoka zizini akampeleka kumnywesha maji siku ya Sabato? 16 Je, huyu mwanamke, ambaye ni binti wa Abrahamu, aliyeteswa na Shetani akiwa amemfunga kwa miaka yote hii kumi na minane, hakustahili kufunguliwa kutoka kifungo hicho siku ya Sabato?"

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    12 Isa alipomwona, akamwita, akamwambia, "Mwanamke, uwe huru, umepona ugonjwa wako." 13 Isa alipomwekea mikono yake, akasimama wima mara moja, akaanza kumtukuza Mungu.

    14 Lakini kiongozi wa sinagogi akakasirika kwa sababu Isa alikuwa ameponya mtu siku ya Sabato. Akaambia umati ule wa watu, "Kuna siku sita ambazo watu wanapaswa kufanya kazi. Katika siku hizo, njooni mponywe, lakini si katika siku ya Sabato."

    15 Lakini Bwana Isa akamjibu, "Enyi wanafiki! Je, kila mmoja wenu hamfungulii ng’ombe wake au punda wake kutoka zizini akampeleka kumnywesha maji siku ya Sabato? 16 Je, huyu mwanamke, ambaye ni binti ya Ibrahimu, aliyeteswa na Shetani akiwa amemfunga kwa miaka yote hii kumi na nane, hakustahili kufunguliwa kutoka kifungo hicho siku ya Sabato?"

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    12 Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. 13 Mk 7:32Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu. 14 Kut 20:9-10;Kum 5:13-14Basi mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu, akawaambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato. 15 Lk 14:5Lakini Bwana akajibu akasema, Enyi wanafiki, kila mmoja wenu, je! Hamfungui ng’ombe wake au punda wake siku ya sabato katika zizi, aende naye kumnywesha? 16 Lk 19:9;Mdo 3:25Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Abrahamu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato?

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.