Publicidade

Lucas 15

20 Basi akaondoka, akaenda kwa baba yake.

"Lakini alipokuwa bado yuko mbali, baba yake akamwona, moyo wake ukajawa na huruma. Akamkimbilia mwanawe, akamkumbatia na kumbusu.

21 "Yule mwana akamwambia baba yake, Baba, nimekosa mbele za Mungu na mbele yako. Sistahili kuitwa mwanao tena.

22 "Lakini baba yake akawaambia watumishi, Leteni upesi joho lililo bora sana, tieni pete kidoleni mwake na viatu miguuni mwake. 23 Leteni ndama aliyenona, mkamchinje ili tuwe na karamu, tule na kufurahi.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-