7 naye akamzaa mwanawe, kifungua mimba. Akamfunika nguo za kitoto na kumlaza katika hori ya kulia ngʼombe, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.
24 na pia kutoa dhabihu kulingana na yale yaliyonenwa katika Sheria ya Bwana: "Hua wawili au makinda mawili ya njiwa."
34 Kisha Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, "Mtoto huyu amewekwa kwa makusudi ya kuanguka na kuinuka kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ambayo watu watanena dhidi yake, 35 ili mawazo ya mioyo mingi yadhihirike. Nao upanga utauchoma moyo wako."