Kubatizwa Kwa Bwana Yesu
21 Baada ya watu wote kubatizwa, Yesu naye akabatizwa. Naye alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka. 22 Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa umbo kama la hua, nayo sauti kutoka mbinguni ikasema: "Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana."