Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 8

Yesu Atuliza Dhoruba

22 Siku moja Yesu alipanda ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, "Tuvukeni twende mpaka ngʼambo ya ziwa." Nao wakaondoka. 23 Hivyo walipokuwa wakienda, akalala usingizi. Dhoruba kali ikatokea mle ziwani, hata mashua ikawa inajaa maji, nao walikuwa katika hatari kubwa.

24 Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, "Bwana, Bwana, tunaangamia!"

Yeye akaamka, akaukemea ule upepo na yale mawimbi; dhoruba ikakoma, nako kukawa shwari. 25 Akawauliza wanafunzi wake, "Imani yenu iko wapi?"

Kwa woga na mshangao wakaulizana, "Huyu ni nani, ambaye anaamuru hata upepo na maji, navyo vikamtii?"

Yesu Amponya Mtu Mwenye Pepo Mchafu

26 Basi wakafika katika nchi ya Wagerasi, ambayo iko upande wa pili wa ziwa kutoka Galilaya.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também