32 Petro na wenzake walikuwa wamelala usingizi mzito. Walipoamka, wakaona utukufu wa Yesu na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye. 33 Mose na Eliya walipokuwa wanaondoka, Petro akamwambia Yesu, "Bwana, ni vizuri tukae hapa! Tutajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Mose na kingine cha Eliya." Lakini Petro alikuwa hajui asemacho.
Publicidade