Gharama Ya Kumfuata Yesu
57 Walipokuwa njiani wakienda, mtu mmoja akamwambia Yesu, "Nitakufuata kokote uendako."
58 Yesu akamjibu, "Mbweha wana mapango, nao ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake."
59 Yesu akamwambia mtu mwingine, "Nifuate."
Mtu huyo akamjibu, "Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu."
60 Yesu akamwambia, "Waache wafu wawazike wafu wao, bali wewe nenda ukautangaze Ufalme wa Mungu."
61 Mtu mwingine akamwambia, "Bwana, nitakufuata lakini naomba kwanza nikawaage jamaa yangu."
62 Yesu akamwambia, "Mtu yeyote atiaye mkono wake kulima, kisha akatazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu."