Pular para o conteúdo
Publicidade

Levítico 18

6 " Hakuna mtu awaye yote atakayemsogelea ndugu wa karibu ili kukutana naye kimwili. Mimi ndimi Bwana.

7 " Usimvunjie heshima baba yako kwa kukutana kimwili na mama yako. Yeye ni mama yako; usiwe na mahusiano kama hayo naye.

8 " Usikutane kimwili na mke wa baba yako; hiyo itamvunjia heshima baba yako.

9 " Usikutane kimwili na dada yako, wala binti wa baba yako, au binti wa mama yako, awe amezaliwa katika nyumba hiyo au mahali pengine.

10 " Usikutane kimwili na binti wa mwanao ama binti wa binti yako; utajivunjia heshima.

11 " Usikutane kimwili na binti wa mke wa baba yako, aliyezaliwa na baba yako; huyo ni dada yako.

12 " Usikutane kimwili na dada wa baba yako; ni ndugu wa karibu wa baba yako.

13 " Usikutane kimwili na dada wa mama yako, kwa sababu ni ndugu wa mama yako wa karibu.

14 " Usimvunjie heshima ndugu wa baba yako, kwa kukutana kimwili na mke wake; yeye ni shangazi yako.

15 " Usikutane kimwili na mkwe wako, yeye ni mke wa mwanao; usiwe na mahusiano kama hayo naye.

16 " Usikutane kimwili na mke wa kaka yako; utamvunjia heshima kaka yako.

17 " Usikutane kimwili na mwanamke kisha na binti yake. Usikutane kimwili na binti wa mwanawe au binti wa binti yake; hao ni ndugu zake wa karibu. Huo ni uovu.

18 " Usimchukue dada wa mke wako kuwa mke mwenza, na kukutana naye kimwili wakati bado mke wako anaishi.

19 " Usimsogelee mwanamke ili kukutana naye kimwili wakati wa unajisi wa siku zake za mwezi.

20 " Usikutane kimwili na mke wa jirani yako na kujitia naye unajisi.

21 " Usimtoe mtoto wako yeyote awe kafara kwa mungu Moleki, kwani hutalinajisi kamwe jina la Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.

22 " Usikutane kimwili na mwanaume kama mtu akutanaye na mwanamke; hilo ni chukizo.

23 " Usikutane kimwili na mnyama na kujitia unajisi kwake. Mwanamke asijipeleke kwa mnyama ili kukutana naye kimwili; huo ni upotovu.

Veja também