Pular para o conteúdo
Publicidade

Mambo Ya Walawi 6:1-5

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Kurudisha Kilichochukuliwa

1 Bwana akamwambia Mose: 2 "Kama mtu yeyote akitenda dhambi, naye si mwaminifu kwa Bwana kwa kumdanganya jirani yake kuhusu kitu fulani alichokabidhiwa, au kimeachwa chini ya utunzaji wake, au kimeibwa, au kama akimdanganya, 3 au akiokota mali iliyopotea na akadanganya, au kuapa kwa uongo, au kama akitenda dhambi yoyote ambayo watu waweza kuitenda; 4 wakati akitenda dhambi hizo na kuwa mwenye hatia, ni lazima arudishe kile alichokuwa amekiiba au amekichukua kwa dhuluma, au alichokuwa amekabidhiwa, au mali iliyokuwa imepotea akaipata, 5 au chochote alichokuwa amekiapia kwa uongo. Lazima akirudishe kikamilifu, na aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, vyote ampe mwenye mali siku ile anapeleka sadaka yake ya hatia.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa: 2 "Mtu yeyote akitenda dhambi, naye si mwaminifu kwa Mwenyezi Mungu kwa kumdanganya jirani yake kuhusu kitu fulani alichokabidhiwa, au kimeachwa chini ya utunzaji wake, au kimeibwa, au kama akimdanganya, 3 au akiokota mali iliyopotea na akadanganya kuihusu, au kuapa kwa uongo, au kama akitenda dhambi yoyote ambayo watu wanaweza kuitenda; 4 wakati akitenda dhambi hizo na kuwa mwenye hatia, ni lazima arudishe kile alichokuwa amekiiba au amekichukua kwa dhuluma, au alichokuwa amekabidhiwa, au mali iliyokuwa imepotea akaipata, 5 au chochote alichokuwa amekiapia kwa uongo. Lazima akirudishe kikamilifu, na aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, vyote ampe mwenye mali siku ile anapeleka sadaka yake ya hatia.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Hes 5:5-8BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2 Hes 5:6;Law 19:11;Mdo 5:4;Kol 3:9;Kut 22:7,10;Mit 24:28;26:19Mtu awaye yote akifanya dhambi, na kuasi juu ya BWANA, akamdanganya mwenziwe katika jambo la amana, au la mapatano, au la kunyang’anya, au kumwonea mwenziwe; 3 Kum 22:1;Law 19:12;Yer 7:9;Zek 5:4;Kut 22:11au kupata kitu kilichopotea na kutenda la uongo juu yake, na kuapa kwa uongo; katika mambo hayo yote mojawapo atakalolitenda mtu, na kufanya dhambi kwalo; 4 ndipo itakapokuwa, akiwa amefanya dhambi, na kupata hatia, atarudisha hicho alichokipata kwa kunyang’anya, au kitu kile alichokipata kwa kuonea, au ile amana aliyowekewa, au kitu kile kilichopotea alichokipata yeye, 5 Law 5:16;Hes 5:7;2 Sam 12:6;Lk 19:8au kitu chochote ambacho amekiapia uongo; atakirudisha hata kwa utimilifu wake, kisha ataongeza na sehemu ya tano zaidi juu yake; naye atampa huyo mwenyewe, siku hiyo ambayo atakapohukumiwa kuwa mwenye hatia.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.