Yesu Amtakasa Mwenye Ukoma
40 Mtu mmoja mwenye ukoma alimjia Yesu, akamwomba akipiga magoti, akamwambia, "Ukitaka, waweza kunitakasa."
41 Yesu, akiwa amejawa na huruma, akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, "Nataka. Takasika!" 42 Mara ukoma ukamtoka, naye akatakasika.