Pular para o conteúdo
Publicidade

Marko 10:28-31

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

28 Ndipo Petro akamjibu, "Tazama, tumeacha kila kitu na kukufuata wewe!"

29 Yesu akasema, "Amin, nawaambia, hakuna mtu yeyote aliyeacha nyumba, ndugu wa kiume au wa kike, au mama au baba, au watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, 30 ambaye hatalipwa mara mia katika ulimwengu huu: nyumba, ndugu wa kiume na wa kike, mama na baba na watoto, mashamba pamoja na mateso, kisha uzima wa milele katika ulimwengu ujao. 31 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na wa mwisho watakuwa wa kwanza."

Yesu Atabiri Mara Ya Tatu Kufa Na Kufufuka Kwake

(Mathayo 20:17-19; Luka 18:31-34)

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    28 Ndipo Petro akamjibu, "Tazama, tumeacha kila kitu na kukufuata wewe!"

    29 Isa akasema, "Amin, nawaambia, hakuna mtu yeyote aliyeacha nyumba, ndugu wa kiume au wa kike, au mama au baba, au watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, 30 ambaye hatalipwa mara mia katika ulimwengu huu: nyumba, ndugu wa kiume na wa kike, mama na baba na watoto, mashamba pamoja na mateso, kisha uzima wa milele katika ulimwengu ujao. 31 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na wa mwisho watakuwa wa kwanza."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    28 Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. 29 Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume, au ndugu wa kike, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, 30 ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu wa kiume, na ndugu wa kike, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele. 31 Mt 20:16;Lk 13:30Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.