Pular para o conteúdo
Publicidade

Marko 10:35-37,41-45

35 Kisha Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakaja kwake na kumwambia, "Mwalimu, tunataka utufanyie lolote tutakalokuomba."

36 Naye akawaambia, "Je, mwataka niwafanyie jambo gani?"

37 Wakamwambia, "Tupe kukaa mmoja upande wako wa kuume na mwingine upande wako wa kushoto katika utukufu wako."

41 Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia hayo, wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana. 42 Lakini Yesu akawaita wote pamoja na kuwaambia, "Mnafahamu kuwa wale wanaodhaniwa kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala watu kwa nguvu, nao wenye vyeo huonyesha mamlaka yao. 43 Lakini isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkuu miongoni mwenu hana budi kuwa mtumishi wenu, 44 na yeyote anayetaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa mtumwa wa wote. 45 Kwa kuwa hata Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi."

Yesu Amponya Kipofu Bartimayo

(Mathayo 20:29-34; Luka 18:35-43)

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.