Yesu Aingia Yerusalemu Kwa Shangwe
1 Walipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage na Bethania katika Mlima wa Mizeituni. Yesu akawatuma wawili wa wanafunzi wake, 2 akawaambia, "Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu. Na hapo mtakapoingia kijijini, mtamkuta mwana-punda amefungwa hapo, ambaye hajapandwa na mtu bado. Mfungueni, mkamlete hapa.
7 Kisha wakamleta huyo mwana-punda kwa Yesu na kutandika mavazi yao juu yake, naye akampanda. 8 Watu wengi wakatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakatandaza matawi waliyokuwa wamekata mashambani. 9 Kisha wale waliokuwa wametangulia mbele na wale waliokuwa wakifuata nyuma wakapaza sauti, wakisema,
"Hosana!"11:9 Kiebrania kusema Okoa, basi likawa neno la shangwe.
"Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!"
10 "Umebarikiwa Ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi!"
"Hosana kwake yeye aliye juu!"
11 Yesu akaingia Yerusalemu na kwenda Hekaluni. Akaangalia kila kitu kilichokuwamo, lakini kwa kuwa ilishakuwa jioni, akaenda zake Bethania pamoja na wale kumi na wawili.
Yesu Alaani Mtini Usiozaa
(Mathayo 21:18-19)