53 Wakampeleka Yesu kwa kuhani mkuu, nao viongozi wa makuhani wote, na wazee na walimu wa sheria wote wakakusanyika pamoja.
55 Viongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi14:55 Baraza la Wayahudi hapa ina maana ya Sanhedrin ambalo lilikuwa ndilo baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi, lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu. lote wakatafuta ushahidi dhidi ya Yesu ili wapate kumuua. Lakini hawakupata jambo lolote. 56 Wengi walitoa ushahidi wa uongo dhidi yake, lakini maelezo yao hayakukubaliana.
61 Lakini Yesu akakaa kimya, hakusema neno lolote.
Kuhani mkuu akamuuliza tena, "Je, wewe ndiwe Kristo,14:61 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Mwana wa Mungu Aliyebarikiwa?"
62 Yesu akajibu, "Mimi ndimi. Nanyi mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni."
63 Kuhani mkuu akararua mavazi yake, akasema, "Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? 64 Ninyi mmesikia hayo makufuru. Uamuzi wenu ni gani?"
Wote wakamhukumu kwamba anastahili kifo.