Pular para o conteúdo
Publicidade

Marko 14:61-64

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

61 Lakini Yesu akakaa kimya, hakusema neno lolote.

Kuhani mkuu akamuuliza tena, "Je, wewe ndiwe Kristo,14:61 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Mwana wa Mungu Aliyebarikiwa?"

62 Yesu akajibu, "Mimi ndimi. Nanyi mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni."

63 Kuhani mkuu akararua mavazi yake, akasema, "Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? 64 Ninyi mmesikia hayo makufuru. Uamuzi wenu ni gani?"

Wote wakamhukumu kwamba anastahili kifo.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    61 Lakini Isa akakaa kimya, hakusema neno lolote.

    Kuhani mkuu akamuuliza tena, "Je, wewe ndiwe Al-Masihi14:61 Al-Masihi maana yake Aliyetiwa mafuta., Mwana wa Mungu Aliyebarikiwa?"

    62 Isa akajibu, "Mimi ndimi. Nanyi mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni."

    63 Kuhani mkuu akayararua mavazi yake, akasema, "Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? 64 Ninyi mmesikia alivyokufuru. Uamuzi wenu ni gani?"

    Wote wakamhukumu kwamba anastahili kifo.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    61 Mk 15:5;Isa 53:7Lakini akanyamaza, wala hakujibu neno. Kuhani Mkuu akamwuliza tena, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wake Mtukufu? 62 Dan 7:13;Zab 110:1Yesu akasema, Mimi ndiye, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kulia wa nguvu, akija na mawingu ya mbinguni. 63 Kuhani Mkuu akararua nguo zake, akisema, Tuna haja gani tena ya mashahidi? 64 Law 24:16;Yn 19:7Mmesikia kufuru yake; mwaonaje ninyi? Wote wakamhukumu kuwa imempasa kuuawa.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.