Pular para o conteúdo
Publicidade

Marko 2:23-28

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

23 Siku moja ya Sabato, Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wakipita katikati ya mashamba ya nafaka. Walipokuwa wakitembea, wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke. 24 Mafarisayo wakamwambia, "Tazama, mbona wanafanya jambo lisilo halali kufanywa siku ya Sabato?"

25 Yesu akawajibu, "Je, hamjasoma kamwe alivyofanya Daudi wakati yeye na wenzake walikuwa na njaa, wakahitaji chakula? 26 Daudi aliingia katika nyumba ya Mungu, wakati Abiathari alikuwa kuhani mkuu, akaila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani peke yao. Naye pia akawapa wenzake."

27 Kisha Yesu akawaambia, "Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, lakini si mwanadamu kwa ajili ya Sabato. 28 Hivyo, Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    23 Siku moja ya Sabato, Isa pamoja na wanafunzi wake walikuwa wakipita katikati ya mashamba ya nafaka. Walipokuwa wakitembea, wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke. 24 Mafarisayo wakamwambia, "Tazama, mbona wanafanya jambo lisilo halali kufanywa siku ya Sabato?"

    25 Isa akawajibu, "Je, hamjasoma alivyofanya Daudi yeye na wenzake walipokuwa na njaa, wakahitaji chakula? 26 Daudi aliingia katika nyumba ya Mungu, Abiathari alipokuwa kuhani mkuu, akaila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani tu. Naye pia akawapa wenzake."

    27 Kisha Isa akawaambia, "Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, lakini si mwanadamu kwa ajili ya Sabato. 28 Hivyo, Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    23 Mt 12:1-8;Lk 6:1-5Ikawa alipokuwa akipita mashambani siku ya sabato, wanafunzi wake walianza kuendelea njiani wakivunja masuke.Kum 23:2524 Mafarisayo wakamwambia, Tazama, mbona wanafanya lisilokuwa halali siku ya sabato? 25 1 Sam 21:1-6Akawaambia, Hamkusoma popote alivyofanya Daudi, alipokuwa akiona njaa na kuhitaji chakula, yeye na wenziwe? 26 Law 24:9Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, wakati Abiathari alipokuwa kuhani mkuu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kuliwa ila na makuhani, akawapa na wenziwe? 27 Kum 5:14Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. 28 Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.