22 Walimu wa sheria walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, "Amepagawa na Beelzebuli!3:22 Beelzebuli kwa Kiyunani ni Beelzebubu, yaani mkuu wa pepo wachafu. Anatoa pepo wachafu kwa kutumia mkuu wa pepo wachafu!"
23 Basi Yesu akawaita na kuzungumza nao kwa mifano akasema: "Shetani awezaje kumtoa Shetani? 24 Kama ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama. 25 Nayo nyumba kama ikigawanyika dhidi yake yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama. 26 Naye Shetani kama akijipinga mwenyewe na awe amegawanyika, hawezi kusimama bali mwisho wake umewadia. 27 Hakuna mtu yeyote awezaye kuingia kwenye nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali zake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu. Ndipo ataweza kuteka nyara mali zake. 28 Amin, nawaambia, dhambi zote na makufuru yote ya wanadamu watasamehewa. 29 Lakini yeyote anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, atakuwa na hatia ya dhambi ya milele."
30 Yesu alisema hivi kwa sababu walikuwa wanasema, "Ana pepo mchafu."