Mama Na Ndugu Zake Yesu
31 Kisha wakaja ndugu zake Yesu pamoja na mama yake. Wakasimama nje, wakamtuma mtu kumwita. 32 Umati wa watu ulikuwa umeketi kumzunguka, nao wakamwambia, "Mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta."
33 Akawauliza, "Mama yangu na ndugu zangu ni nani?"
34 Kisha akawatazama wale watu waliokuwa wameketi kumzunguka pande zote, akasema, "Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu. 35 Mtu yeyote anayetenda mapenzi ya Mungu, huyo ndiye ndugu yangu, na dada yangu na mama yangu."