Pular para o conteúdo
Publicidade

Marko 5

Yesu Amfufua Binti Yairo

35 Alipokuwa bado anaongea, watu wakafika kutoka nyumbani kwa Yairo. Wakamwambia, "Binti yako amekufa. Kwa nini kuendelea kumsumbua Mwalimu?"

36 Aliposikia hayo waliyosema, Yesu akamwambia huyo kiongozi wa sinagogi, "Usiogope. Amini tu."

37 Hakumruhusu mtu mwingine yeyote amfuate isipokuwa Petro, Yakobo na Yohana, nduguye Yakobo. 38 Walipofika nyumbani kwa yule kiongozi wa sinagogi, Yesu akaona ghasia, watu wakilia na kuomboleza kwa sauti kubwa. 39 Alipokwisha kuingia ndani, akawaambia, "Kwa nini mnafanya ghasia na kulia? Mtoto hajafa, bali amelala tu." 40 Wale watu wakamcheka kwa dharau.

Lakini yeye akawatoa wote nje, akawachukua baba na mama wa yule mtoto, pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao. Wakaingia ndani mpaka pale alipokuwa yule mtoto. 41 Akamshika mtoto mkono, akamwambia, "Talitha koum!" 5:41 Talitha koum ni lugha ya Kiaramu. (maana yake ni, "Msichana, nakuambia: amka!") 42 Mara yule msichana akasimama, akaanza kutembea (alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili). Walipoona haya, wakastaajabu sana. 43 Yesu akawaagiza kwa ukali wasimweleze mtu yeyote jambo hilo, naye akawaambia wampe yule msichana chakula.

Veja também