Pular para o conteúdo
Publicidade

Marko 6:1-6

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Nabii Hana Heshima Kwao

1 Yesu akaondoka huko na kwenda mji wa kwao, akiwa amefuatana na wanafunzi wake. 2 Ilipofika siku ya Sabato, akaanza kufundisha katika sinagogi, na wengi waliomsikia wakashangaa.

Nao wakauliza, "Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya yote? Tazama ni hekima ya namna gani hii aliyopewa? Tazama matendo ya miujiza ayafanyayo kwa mikono yake! 3 Huyu si yule seremala, mwana wa Maria? Na ndugu zake si Yakobo, Yose,6:3 Yosefu kwa Kiyunani ni Joses. Yuda na Simoni? Dada zake wote si tuko nao hapa kwetu?" Nao wakachukizwa sana kwa ajili yake, wakakataa kumwamini.

4 Yesu akawaambia, "Nabii hakosi heshima isipokuwa katika mji wake mwenyewe, na miongoni mwa jamaa na ndugu zake, na nyumbani kwake." 5 Hakufanya miujiza yoyote huko isipokuwa kuweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache na kuwaponya. 6 Naye akashangazwa sana kwa jinsi wasivyokuwa na imani.

Yesu Awatuma Wale Kumi Na Wawili

(Mathayo 10:5-15; Luka 9:1-6)

Kisha Yesu akawa anakwenda kutoka kijiji kimoja hadi kingine akifundisha.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Isa akaondoka huko na kwenda mji wa kwao, akiandamana na wanafunzi wake. 2 Ilipofika siku ya Sabato, akaanza kufundisha katika sinagogi, na wengi waliomsikia wakashangaa.

    Nao wakauliza, "Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya yote? Tazama ni hekima ya namna gani hii aliyopewa? Tazama matendo ya miujiza ayafanyayo kwa mikono yake! 3 Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu? Na ndugu zake si Yakobo, Yose6:3 yaani Yusufu, Yuda na Simoni? Dada zake wote si tuko nao hapa kwetu?" Nao wakachukizwa sana kwa ajili yake, wakakataa kumwamini.

    4 Isa akawaambia, "Nabii hakosi heshima isipokuwa katika mji wake mwenyewe, na miongoni mwa jamaa na ndugu zake, na nyumbani mwake." 5 Hakufanya miujiza yoyote huko isipokuwa kuweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache na kuwaponya. 6 Naye akashangazwa sana kwa kutoamini kwao.

    Kisha Isa akawa anaenda kutoka kijiji kimoja hadi kingine akifundisha.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Mt 13:53-58;Lk 4:15-30Akatoka huko, akafika mpaka nchi ya kwao; wanafunzi wake wakamfuata. 2 Yn 7:15Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? 3 Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na dada zake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. 4 Yn 4:44Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani mwake. 5 Mk 6:13Wala hakuweza kufanya mwujiza wowote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya.

    6 Akastaajabu kwa sababu ya kutoamini kwao. Akazungukazunguka katika vile vijiji, akifundisha.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.