Publicidade

Marcos 6

35 Mchana ulipokuwa umeendelea sana, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, "Mahali hapa ni nyikani, nazo saa zimekwenda sana. 36 Waage watu ili waende mashambani na vijijini jirani, wakajinunulie chakula."

37 Lakini Yesu akawajibu, "Ninyi wapeni chakula."

Wakamwambia, "Je, twende tukanunue mikate ya dinari 2006:37 Dinari moja ilikuwa kama mshahara wa kibarua wa siku moja; hivyo dinari 200 ni sawa na mshahara wa siku 200. ili tuwape watu hawa wale?"

38 Akawauliza, "Kuna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie."

Walipokwisha kujua wakarudi, wakamwambia, "Kuna mikate mitano na samaki wawili."

39 Kisha Yesu akawaamuru wawaketishe watu makundi makundi kwenye majani, 40 nao wakaketi kwenye makundi ya watu mia mia na wengine hamsini hamsini. 41 Yesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi wake ili wawagawie wale watu wote. Pia akawagawia wote wale samaki wawili. 42 Watu wote wakala, wakashiba. 43 Nao wanafunzi wake wakakusanya vipande vilivyosalia vya mikate na samaki, wakajaza vikapu kumi na viwili. 44 Idadi ya wanaume waliokula walikuwa 5,000.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-