48 Akawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Yesu akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita, 49 lakini walipomwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu. Wakapiga yowe, 50 kwa sababu wote walipomwona waliogopa.
Mara Yesu akasema nao, akawaambia, "Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!" 51 Akapanda ndani ya mashua nao, na ule upepo ukakoma! Wakashangaa kabisa,