Pular para o conteúdo
Publicidade

Marko 8

Yesu Amponya Kipofu Huko Bethsaida

22 Wakafika Bethsaida na baadhi ya watu wakamleta mtu mmoja kipofu wakamsihi Yesu amguse. 23 Yesu akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Yesu akamuuliza, "Unaona chochote?"

24 Yule kipofu akaangalia, akasema, "Ninaona watu, wanaonekana kama miti inayotembea."

25 Yesu akamwekea tena mikono machoni. Kisha macho yake yakafunguka, kuona kwake kukarejea naye akaona kila kitu dhahiri. 26 Yesu akamuaga aende nyumbani kwake, akimwambia, "Hata kijijini usiingie."

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também