Pular para o conteúdo
Publicidade

Malaki 3:7-11

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

7 Tangu wakati wa baba zenu mmegeukia mbali na amri zangu nanyi hamkuzishika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi," asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

"Lakini mnauliza, ‘Tutarudi kwa namna gani?’

8 "Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Hata hivyo mnaniibia mimi.

"Lakini mnauliza, ‘Tunakuibia kwa namna gani?’

"Mnaniibia zaka na dhabihu. 9 Mko chini ya laana, ninyi taifa lote, kwa sababu mnaniibia mimi. 10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kuwe na chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili," asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, "nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha. 11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu, wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake," asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    7 Tangu wakati wa baba zenu mmegeukia mbali na amri zangu nanyi hamkuzishika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi," asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.

    "Lakini mnauliza, ‘Tutarudi kwa namna gani?’

    8 "Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Hata hivyo mnaniibia mimi.

    "Lakini mnauliza, ‘Tunakuibia kwa namna gani?’

    "Mnaniibia zaka na dhabihu. 9 Mko chini ya laana, ninyi taifa lote, kwa sababu mnaniibia mimi. 10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kuwe na chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili," asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, "nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi hata mkose nafasi ya kutosha. 11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu, wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake," asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    7 Mdo 7:51;Kum 30:1-4;Isa 55:6,7;Zek 1:3Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?

    8 Neh 13:10Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. 9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. 10 Mit 3:9;1 Nya 26:20;Mwa 7:11;Law 27:30;Hes 18:21-24;Kum 12:6;14:22-29;Neh 13:12Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. 11 Amo 4:9Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Malaquias
Ver todos os capítulos de Malaquias